Operesheni Firat inaarifiwa kuingia katika
siku ya 14 huku kikosi cha jeshi la Uturuki (TSK) kikiendeleza harakati
dhidi ya ugaidi.Vifaru viwili vya kijeshi vinavyomilikiwa na TSK
vimeripotiwa kushambuliwa kwa roketi na mapigano kuzuka kati ya
wanajeshi na DAESH katika eneo la Wakuf.
Askari watatu mashujaa wameripotiwa kupoteza maisha na wengine wanne kujeruhiwa kwenye mashambulizi hayo.
Ngome 50 za magaidi ziliweza kugunduliwa na kulengwa na kikosi cha TSK kwa makombora 225 yaliyorushwa.
Tangu kuanzishwa kwa operesheni hiyo hadi kufikia sasa, ngome 443 za magaidi zimeweza kulengwa kwa makombora 1,924 yaliyorushwa.
Wakati huo huo, vikosi vya wapiganaji wa upinzani pia vimeripotiwa kuidhibiti miji ya Wakuf na Sadwi kutoka mikononi mwa magaidi.

0 comments:
Post a Comment