Kwa kawaida kila mwanamke hupitia hali ya kupatwa na hedhi kila mwezi,
ikiwa ni hali yao ya kawaida kutokana na Mungu alivyowaumba.
Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wanapokuwa ndani ya siku hizo.
Ufuta
Ufuta ni mbegu za asili ambazo huweza kutumika kwa kupunguza maumivu
wakati wa hedhi, unachopaswa kufanya ni kusaga ufuta kisha tumia unga
wake na utakusaidia.
Tangawizi
Kiungo hiki nacho husaidia kupunguza maumiwa ya wakati wa hedhi, unaweza
kutumia siku mbili kabla ya kuingia katika mzunguko wako ili kupata
matokeo mazuri zaidi.
Papai
Papai hususani lile bichi pia huweza kuwa moja ya suluhisho ya tatizo ya
maumivu wakati wa hedhi kwani husaidia kulainisha misuli ya sehemu za
uzazi na hivyo kusaidia kupunguza maumivu wakati wa hedhi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment