Shida ni kwamba wanawake wengi wanatatizo hili na wameona kama ni hali
ya kawaida kabisa, huku wasijue nini cha kufanya hivyo leo nimeona
tujuzane hizi mbinu za kuweza kukusaidia kuondokana na hali hiyo.
Tatizo la kimahusiano kati ya mwaume na mwanamke.
Kwa kawaida ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga
ndoa. Ikiwa uhusiano haupo vizuri ni rahisi ndoa hiyo kuingia katika
matatizo. Mwanamke anaweza kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
Matatizo ya kisaikolojia. Ikiwa
mwanamke ana matatizo ya kisaikolojia ni rahisi kumfanya mwanamke akose
hamu ya kushiriki tendo la ndoa, kwakuwa tendo la ndoa huwa ni hisia na
huanzia akili na hivyo utulivu wa fikra ni muhimu ili mwanamke huyu
aweze kulifurahia tendo la ndoa.
Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
Mwanamke mwenye matatizo ya kifedha au kikazi na yakamfanya afikiri sana
juu ya matatizo hayo kuliko mambo mengine ya kimaendeleo ni rahisi
mwanamke huyu kukumbwa na tatizo hili la kukosa hamu ya kushiriki tendo
la ndoa.
Manyanyaso ya kijinsia
Mwanamke mwenye historia ya kunyanyaswa kijinsia huathirika
kisaikolojia. Mwanamke aliyebakwa au kukeketwa anaweza kakosa hamu ya
kushiriki tendo la ndoa kwani tayari akilini anakuwa anajeraha
linalomfanya asione raha ya kushiriki katika tendo la ndoa.
Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
Ikiwa mwanamke akidharauliwa na akajua anadharauliwa na jamii ni rahisi
kuathirika kisaikolojia na hivyo kupelekea kukumbwa na tatizo hili la
kukosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa.
0 comments:
Post a Comment