Kila mtu hupenda kuwa na afya njema wakati wote ili kuweza kuendelea na mikakati ya kila siku ya kuendesha maisha.
Hapa ninazo baadhi ya kanuni ambazo zikifuatwa vizuri huweza kukusaidia kuwa na afya njema siku zote.
Hewa safi
Hewa safi ni muhimu wakati wote iwe mchana au usiku, hivyo hakikisha
nyumba yako au mahali pako pa kazi kuna mazingira ambayo yanaruhusu
uwepo wa hewa safi muda wote.Hewa safi husaidia damu kuzunguka vizuri
mwilini kutokana na kuwa na kiwango cha kutosha cha oksijeni.
Kupata muda wa kupumzika
Kwa kawaida mwili ni muhimu kupumzika kutokana na msongo wa majukumu ya kila siku
Mazoezi
Mazoezi nayo ni muhimu sana kwa afya zetu ikiwa ni pamoja na kuulinda
mwili dhidi ya magonjwa yasiyoyakuambukiza, pia mazoezi husaidia kufanya
mzunguko wa damu kuwa mzuri ndani ya mwili pamoja na kukufanya kuwa na
uwezo mzuri na wa haraka katika kufanya maamuzi.
Maji
Inatupaswa kunywa maji ya kutosha kutokana na maji kuwa na umuhimu
mkubwa kwa kila seli ndani ya mwili. Karibia asilimia 70 ya miili yetu
ni maji hivyo inaonesha ni kwa kiasi gani maji yanaumuhimu kwa afya
zetu.
Lishe bora.
Wataalam wa lishe bora wamekuwa wakishauri matumizi ya chakula cha awali
yaani nafaka, kokwa, matunda na mbogamboga. Ukitaka kuanza kula vyakula
vya mimea hakikisha unafahamu vizuri namna ya kuandaa lishe bora.
Epuka vitu vyenye madhara
Mfano wa vitu hivyo ni sigara, dawa za kulevya pombe nk.Ni vyema
ukatambua kuwa matumizi ya pombe huathiri mfumo mzima wa kinga za mwili
na kuufanya kuwa dhaifu.Pia huchangia kudhoofisha mfumo mzima wa uzazi
kwa jinsia zote mbili.
Kumuamini Mungu
Watu wengi wambao husimama katika imani zao Mungu huwasaidia na kulinda afya zao mara zote.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment