Image
Image

Balozi wa Marekani aituhumu Urusi kwa kuzungumza uongo.

Balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa, Samantha Power ameituhumu Urusi kwa kuzungumza uongo uliodhahiri kuhusiana na uwepo wa Majeshi yake nchini Syria.
Bi.Power amesema kuwa Warusi hawakushirikishwa katika kupambana na ugaidi nchini Syria lakini  wapo nchini humo wakifanya harakati za kijeshi kinyume na utaratibu.
Amelieleza  baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba Urusi na Syria wanatekeleza vitendo vyote vya kimabavu dhidi ya upinzani uliopo Mashariki mwa mji wa Alepo.
Kwa upande mwingine Balozi wa Urusi katika umoja huo, Vitaly Churkin, amewatuhumu waasi kwa kuvunja makubaliano ya kusitisha vita ambayo yalishindikana ndani ya muda mchache tu.
Naye Mwakilishi wa Syria ameliambia baraza hilo la usalama kwamba jimbo lote la Alepo litarudishwa mikononi mwa serikali  ya nchi hiyo siku chache zijazo.
Mji wa Allepo kwa sasa umekuwa kitovu cha mapigano yanayoendelea nchini Syria baina ya pande zinazokinzana nchini humo hali iliyosababisha huduma za kijamii kukosekana katika mji huo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment