Dawa
ya kwanza duniani ya kutibu ugonjwa wa kifua kikuu miongoni mwa watoto
inatarajiwa kuzinduliwa leo siku ya Jumanne mjini Nairobi.
Hadi kufikia sasa,watoto hutumia dawa zinazotumiwa na watu wazima ambazo hugawanywa kusagwa na kutiwa katika maji.
Daktari
Cherise Scott,mkurugenzi wa maswala ya magonjwa ya watoto katika
muungano wa utengezaji wa dawa za TB ,anasema kuwa dawa hiyo mpya
inaweza kuleta afueni kwa watoto milioni moja ambao huambukizwa kifua
kikuu kila mwaka ,pamoja na waangalizi wao.
Kenya ndilo taifa la
kwanza kutoa dawa hiyo mpya kwa raia wake huku mataifa zaidi
yakitarajiwa kuendelea na utoaji wa dawa hizo katika kipindi cha miaka
mitatu ijayo.
Dawa hiyo ni mchanganyiko wa dawa tatu zinazotumiwa
kutibu Tb,zikiwa zimechanganywa kikamilifu na kuwekwa ladha ili
kuwavutia watoto.
Inaweza kuyayuka kwa urahisi ndani ya maji,hivyobasi kuifanya kuwa rahisi kutumia kila siku katika kipindi cha miezi sita.
Hadi
kufikia sasa ,waangalizi wa watoto hulazimika kuzivunja dawa hizo kabla
ya kuwapatia watoto hao.Dawa hizo ambazo ziko uchungu ni vigumu kumeza.
Ugonjwa wa kifua kikuu unaongoza miongoni mwa magonjwa hatari dunia,na huwaua watu 3000 kila siku.
Dawa hiyo mpya itayasaidia maisha ya watoto zaidi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment