Mgogoro
ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) bado unafukuta ambapo jana Prof.
Ibrahim Lipumba, aligomea mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la chama
hicho ulioitishwa leo visiwani Zanzibar
Alisema, taarifa zilizotolewa
kwa vyombo vya habari kuhusu kufanyika kwa mkutano huo hazitambui kwa
kuwa, mamlaka zinazohusika kuitisha kikao hicho hazijakidhi matakwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini
Dar es Salaam kupitia taarifa iliyoandaliwa na Magdalena Sakaya, Naibu
Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa na chama hicho alisema, matakwa ya
katiba hayakuzingatiwa.
“Wajibu wa Kamati ya Utendaji ya Taifa
utakuwa kuandaa.. agenda za Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na
kutayarisha na kuhifadhi mihtusari ya vikao vyote vya Mkutano Mkuu wa
Taifa, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na vya kamati ya utendaji ya taifa
yenyewe na kuwasilisha taarifa ya yatokanayo kutokana na utekelezaji wa
maamuzi ya kikao kilichohusika kilichopita,” Prof. Lipumba amenukuu
katiba ya chama hicho ibara ya 85(5).
Prof. Lipumba alisema, Maalim
Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho yupo nje ya nchi na
kwamba, kutokana na Katiba ya CUF,Naibu Katibu Mkuu atakayemfuata Katibu
Mkuu kwa madaraka ni yule aliyetoka upande tofauti wa Jamhuri ya
Muungano na upande anaotoka Katibu Mkuu
Kwa upande wake Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa alisema;
"Mimi
sijaitisha wala sina taarifa ya kikao cha kamati ya utendaji
kilichofanyika Zanzibar, kwa taarifa nilizonazo hakuna wajumbe wa kamati
ya utendaji kutoka Bara waliokua Zanzibar wakati wa kikao hicho.
Nachukua nafasi kuwajulisha wajumbe wote wa baraza kuu kuwa hakuna kikao
chochote cha baraza kuu kilichoandaliwa na kamati ya utendaji ya Taifa
ambayo kikatiba mimi ndiye mwenyekiti wake wakati katibu mkuu hayupo.
“Mimi
ndiye mwenye mamlaka ya Katibu Mkuu kwa sababu Naibu Katibu Mkuu wa CUF
Tanzania Bara kikatiba ndiye msimamizi namba moja wa Katibu Mkuu” .
Alisema,
Katiba ya CUF ya mwaka 1992 Toleo la 2014 kifungu cha 95 (3) kinaeleza
“Naibu Katibu Mkuu atakayemfuata Katibu Mkuu kwa madaraka ni yule
aliyetoka upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande anaotoka
Katibu Mkuu,” na kwamba, Katibu Mkuu anatoka Zanzibar na yeye anatoka
Bara.
Hata hivyo Prof. alisisitiza kuwa, Sakaya hana taarifa ya kikao hicho cha kamati tendaji kilichofanyika Zanzibar.
Pamoja
na kuwepo kwa sintofahamu kutokana na uamuzi wa Jaji Mutungi kumtambua
Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho, (Lipumba)
amepongeza kurejeshwa kwake.
Prof. Lipumba, mwenyekiti wa chama hicho
aliyesimamishwa na CUF mwezi uliopita, alirejea kwenye nafasi hiyo kwa
kauli ya Jaji Mutungu, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Prof.
Lipumba alieleza kushangazwa na hatua ya Jaji Mutungi kukosolewa na
baadhi ya wanasheria na majaji mashuhuri kuwa, hakuna sheria inayompa
furasa jaji huyo kuchukua hatua aliyoichukua.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment