Image
Image

IGP Mangu kukabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika.




Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu anatarajia kukabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) katika mkutano unaotarajiwa kufanyika tarehe 16 Septemba, 2016 jijini Arusha. IGP Mangu atakabidhiwa uenyekiti huo kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi ya Msumbiji ambapo atadumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa kamati tendaji za SARPCCO amabazo zitakutana Septemba 14 na 15 mwaka huu  ili kuandaa ajenda na mapendekezo  ambayo yatawasilishwa katika mkutano wa wakuu wa Polisi ambao unatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Katika mkutano huo mambo mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu yatajadiliwa ikiwemo uhalifu wa kuvuka mipaka, pamoja na kuweka mikakati na maazimio ya  kufanya Oparesheni za pamoja zinazojumuisha nchi zinazounda shirikisho hilo.
Vilevile, mkutano huo utajadili kwa kina utekelezaji wa maazimio mbalimbali kupitia kamati tendaji za wakurugenzi  wa upelelezi, kamati tendaji ya sheria, kamati tendaji ya mafunzo na kamati tendaji ya mtandao wa Polisi wanawake.
Aidha, suala la michezo baina ya Majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama nalo litajadiliwa katika mkutano huo.
SARPCCO iliundwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika katika kukabiliana na uhalifu. Mpaka hivi sasa umoja huo unaundwa na Nchi kumi na tano ambazo ni Tanzania, Angola, Botswana, Malawi, Lesoto, Mauritius, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC), Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Madagascar na Seychelles.
Imetolewa na:-
Advera John Bulimba – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment