Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo
8-Sep-2016 mjini Mtwara wakati
anafungua jengo la sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini
ambalo ujenzi wake umegharimu takribani shilingi bilioni MBILI.
Makamu wa Rais amesema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa
haraka zitakomesha na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na
watumishi wa umma hali ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni
watendaji hao.
Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuiimarisha
sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini kwa kuijengea uwezo wa
rasilimali watu na fedha kwa kadri hali ya uchumi itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza
majukumu yao kwa ufanisi.
Makamu wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi wa
umma kuthamini na wahakikishe walinda maslahi ya umma wakati wote wa utendaji
wao wa kazi ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.
Makamu wa Rais amesema ni jambo la muhimu kwa
sekretarieti hiyo kufutilia mienendo ya viongozi wa umma na kuwabaini wale
wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla
hawaleta madhara kwa serikali na jamii kwa ujumla.
Makamu wa Rais pia ametoa rai maalum kwa wananchi wa
mkoa wa Mtwara kuitumia ofisi hiyo mpya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi
wa umma Kanda ya Kusini kwa kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi
wanaokiuka maadili ya umma katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa
hatua.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki amesisitiza kuwa
kazi ya kuhakiki mali na madeni ya viongozi wa umma itaendelea kwa kasi nchini
na mwaka huu sekretarieti hiyo itahakiki mali za viongozi wapatao 500 kote
nchini.
Naye Jaji Mstaafu na Kamishna wa Maadili Nchini
Salome Kaganda akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo ameiomba serikali
itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na
madeni ya viongozi kwa nchi nzima.
Imetolewa
na
Ofisi
ya Makamu wa Rais
Mtwara.
8-Sep-2016.
0 comments:
Post a Comment