MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekataa maombi ya Wakili wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) ya kuwazuia waandishi wa habari wasiandike kesi inayohusu
utekelezaji wa amri iliyoitaka benki hiyo kulipa Sh bilioni 92.
Jaji
Ama Munisi ametoa uamuzi huo baada ya Wakili wa Benki hiyo, Karim
Rashid kudai kuwa kesi hiyo inasikilizwa faragha hivyo watu wengine
wakiwemo waandishi hawaruhusiwi kusikiliza.
“Naona kuna watu
wanaandikaandika humu ndani na wakati tunajitambulisha,
hawajajitambulisha pia shauri hili linasikilizwa chamber (faragha)
hapaswi mtu mwingine kusikiliza isipokuwa wahusika.” alisema Wakili
Rashid.
Jaji Munisi amesema ingawa wanasikiliza kwenye chumba cha
faragha, suala hilo lipo wazi na kesi hiyo si ya faragha, hivyo ni
ruhusa mtu yeyote kuingia na kusikiliza.
Kesi hiyo ilitajwa leo kwa
ajili ya kusikiliza pingamizi la Kampuni ya Coast Textiles Ltd kupinga
maombi ya kusitisha utekelezaji wa amri ya kulipa fedha hizo
yaliyowasilishwa na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Profesa Benno
Ndulu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment