Mahakama kuu ya Israel imekataa ombi la dhamana lililowasilishwa na
waziri mkuu wa zamani Ehud Olmert aliyekutwa na hatia ya kuhusika na
ufisadi.Kulingana na taarifa za kituo cha redio cha Israel,
iliarifiwa kwamba Olmert ameongezewa miezi 8 zaidi kwenye hukumu ya
kifungo cha miezi 19 aliyopewa hapo awali na mahakama.
Kufuatia uamuzi wa mahakama kuu wa kukataa dhamana, Olmert atalazimika kutumikia kifungo cha miaka 2 na miezi 3 gerezani.
Baada
ya kukabiliwa na kashfa ya ufisadi, Olmert alitupwa gerezani na kuanza
kutumikia kifungo cha miezi 19 tangu mwezi Februari mwaka huu.
Kesi
hiyo iliibuka baada ya Olmert kudaiwa kupokea rushwa kwa ajili ya mradi
wa Holyland Park wakati alipokuwa akihudumu kama meya wa manispaa ya
mji wa Jerusalem.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment