Raia wa Burundi wamefanya maandamano ya kupinga ripoti ya UN iliyochapishwa kuhusiana na ukiukaji wa haki za kibinadamu.Mamia
ya Warundi walikusanyika katika mji mkuu wa Bujumbura na kuikashifu
ripoti ya UN iliyotoa madai ya ukiukaji wa haki za kibinadamu na
tahadhari ya mauaji ya halaiki nchini humo.
Waandamanaji hao walioandamana mbele ya jengo la UN, walitoa maelezo na kuikosoa ripoti hiyo iliyoshindwa kubainisha wazi hali halisi ya Burundi.
Mnamo tarehe 19 Septemba, UN ilichapisha ripoti iliyobainisha kuendelezwa kwa ukiukaji wa haki za kibinadamu ingawaje viongozi wa serikali wanaodaiwa kuhusika wameshindwa kuchukuliwa hatua.

0 comments:
Post a Comment