Image
Image

Jolie atoa wito wa utatuzi wa mzozo wa Syria.


Mwigizaji maarufu wa Hollywood Angelina Jolie ambaye pia ni balozi wa UN wa kutetea haki za wakimbizi, alitekeleza ziara ya kambi ya El-Ezrak iliyoko nchini Jordan.
Jolie alitoa maelezo kwa wanahabari baada ya kutekeleza ziara hiyo na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa Syria.
Katika maelezo yake Jolie alisema, ‘‘Hakuna familia isiyokuwa na matatizo ndani ya kambi hii. Kuna watoto wadogo wanaokabiliwa na ugumu wa maisha. Nasikitika kuona hali hii.’’
Tangu kuibuka kwa mzozo wa Syria, Jolie ameweza kuzuru kambi hiyo nchini Jordan kwa mara ya 4.
Jolie alilaumu viongozi wa dunia kwa kushindwa kutatua mzozo wa Syria ili kuzuia ongezeko la idadi ya wakimbizi.
Kulingana na takwimu zilizotolewa, imebainishwa kuwepo kwa wakimbizi 390,000 wa Syria wanaotafuta hifadhi katika eneo la mpakani mwa Jordan na Syria lililoko umbali wa kilomita 375.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment