Image
Image

Emmanuel Wani auawa Sudan Kusini baada ya kuripoti kesi za ukiukaji wa haki za kibinadamu kwa UN


Emmanuel Wani ambaye ni mwanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu nchini Sudan Kusini, ameripotiwa kuuawa siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa Juba.
Emmanuel Wani anadaiwa kuuawa wiki moja baada ya kuripoti kesi za ukiukaji wa haki za kibinadamu kwa baraza la usalama la UN kama vile ubakaji unaotekelezwa na wanajeshi wa serikali.
Emmanuel Wani pamoja na wanaharakati wenzie walikukatana na wajumbe 15 wa baraza la usalama la UN lililoongozwa na wawakilishi wa Marekani wiki iliyopita mjini Juba.
Wajumbe hao walikuwa wakijadili suala la usalama na kushawishi serikali ya Sudan Kusini kukubali uamuzi wa kutumwa kwa majeshi ya amani nchini humo.
Mmoja wa wanaharakati Edmond Yakani alielezea wanahabari wa AA kwamba Emmanuel Wani aliuawa wiki moja baada ya mkutano wao na wajumbe wa baraza la usalama la UN.
Vyanzo vya habari vinaarifu kwamba baadhi ya wanaharakati wamelazimika kutorokea nje ya nchi baada ya mauaji hayo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment