Majaji hao pia wamemhimiza waziri wa elimu kushauriana na viongozi wa taasisi za taalum ili kuhakikisha uhuru na haki ya dini haikiukwi wala ubaguzi kutokea.
Jopo la majaji lililoongozwa na mwanasheria Phillip Waki wa mahakama kuu ya rufaa, lilifutilia mbali pendekezo la kuweka marufuku ya vazi la hijab hasa mashuleni.
Majaji hao pia walitoa wito kwa walimu kutofanya ubaguzi wa aina yoyote dhidi ya wanafunzi kwa misingi ya mavazi yao wala imani zao za kidini.
Kwa upande mwengine, Kadhi Mkuu wa Kenya Hammad Mohammed Kassim alitoa maelezo na kusisitiza kwamba vazi la hijab ni mojawapo ya masharti kwa wanawake wa Kiislamu.


0 comments:
Post a Comment