Hundi ya fedha
hizo imekabidhiwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam na Balozi wa India hapa nchini
Mhe. Sandeep Arya na baadaye Rais Magufuli akaikabidhi kwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa.
Katika barua yake
kwa Rais Magufuli iliyosomwa na Balozi Sandeep Arya, Waziri Mkuu wa India Mhe.
Narendra Modi amesema Serikali na Wananchi wa India wamepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za kutokea kwa maafa hayo yaliyosababisha vifo vya watu na
uharibifu wa mali.
"Tunaziombea
amani na uvumilivu familia zote zilizopatwa na madhara na pia tunapenda
kuwahakikishia kuwa tupo pamoja na marafiki zetu Serikali ya Tanzania katika
kipindi hiki kigumu" amesema Waziri Mkuu
Modi.
Kwa Upande wake
Rais Magufuli amemshukuru Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi na Serikali
yake kwa kutoa mchango huo na kutuma salamu za rambirambi, na amesema Serikali
yake imeguswa na moyo wa upendo waliounesha.
"Mhe. Balozi
Sandeep Arya naomba unifikishie shukrani zangu za dhati kwa Waziri Mkuu Mhe.
Narendra Modi, mwambie kwa niaba ya Serikali yangu tunamshukuru sana kwa kutoa
msaada huu muhimu kwa ajili ya Watanzania wenzetu waliopatwa na maafa kule
Kagera.
"Mwambie
ameonesha moyo wa upendo na ushirikiano kwetu na tumefarijika kwamba marafiki
zetu mmeguswa kwa namna ya kipekee na tatizo lililoipata nchi yetu"
amesema Rais Magufuli.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Bukoba Bw. Steven Makonda baada ya kubaini kuwa wamefungua akaunti
nyingine ya benki kwa kutumia jina linalofanana na akaunti rasmi ya kuchangia
maafa iitwayo "Kamati Maafa
Kagera" kwa lengo la kujipatia fedha.
Taarifa
iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa muda mfupi baada ya kupokea hundi ya msaada kutoka kwa Waziri Mkuu wa
India imeeleza kuwa pamoja na kutengua uteuzi huo Rais Magufuli ameagiza vyombo
vya dola vichukue hatua dhidi ya wote waliohusika katika njama za kufungua akaunti
hiyo.
Aidha, Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw.
Simbaufoo Swai kutokana na kuhusika katika njama hizo.
Hata hivyo Mhe.
Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuendelea kuchangia
misaada kwa ajili ya walioathirika kwa kutumia akaunti rasmi ya "Kamati Maafa Kagera" ambayo
imetangazwa na Serikali.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
27
Septemba, 2016
0 comments:
Post a Comment