COLOMBIA na waasi wa watiliana saini mkataba wa amani.
Serikali ya COLOMBIA na waasi wa wametiliana saini mkataba wa amani wa kumaliza mapigano yaliyodumu kwa miongo MITANO nchini humoMakataba huo wa kihistoria umetiwa saini na Rais wa COLOMBIA JUAN MANUEL SANTOS na kiongozi wa waasi wa FARC TIMOLEON JIMENEZ.
Zaidi ya watu 2500 wakiwepo watu mashuhuri wamehudhuria ghafla hiyo akiwemo rais wa CUBA, RAUL CASTRO ambaye alikuwa msuluhishi wa mgogoro huo kwa kipindi cha miaka MINNE tangu mwaka 2012.
Rais wa COLOMBIA, MANUEL SANTOS amesema mkataba huo wa amani na kundi la waasi wa FARC utasaidia kukuza uchumi wa nchi hiyo uliozorota kwa muda mrefu.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vimedumu nchini COLOMBIA kwa miaka 42 ambapo maelfu ya watu wamepoteza maisha. Kura ya maoni itafanyika wiki ijayo kuhusiana na mchakato huo wa amani.
0 comments:
Post a Comment