Image
Image

CUF watumie busara kumaliza mpasuko

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimekumbwa na mpasuko, baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kumrejesha Mwenyekiti aliyejiuzulu, Profesa Ibrahim Lipumba na wanachama kadhaa ambao walivuliwa uanachama, wakiwamo wabunge wawili.

Jaji Mutungi alitangaza uamuzi huo mwishoni mwa wiki, akisema uamuzi wa kikao cha Baraza Kuu la Uongozi wa Agosti 29 ulikiuka katiba ya CUF.
Wabunge waliovuliwa uanachama wa chama hicho ni Maftaha Abdallah Nachuma wa Jimbo la Mtwara Mjini na Magdalena Hamis Sakaya wa Jimbo la Kaliua. Wabunge hao walivuliwa uanachama kutokana na kuunga mkono vurugu zilizotokea wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho uliofanyika Dar es Salaam Agosti 27.
Maftaha Abdallah Nachuma alisimamishwa kwa muda usiojulikana na wanachama wengine akiwamo Profesa Lipumba.
Kwa ujumla matukio kadhaa yaliyotokea kabla na baada ya Jaji Mutungi kumrejesha Lipumba ofisini, yanaashiria kuwapo kwa mpasuko mkubwa ambao unahitajika kutafutiwa ufumbuzi wa haraka kabla yaijasababisha athari zaidi.
Viashiria vya mpasuko huo vilianza kuonekana wakati wa Mkutano Mkuu maalumu uliofanyika jijini Dar es Salaam Agosti 27, mwaka huu lengo lake likiwa pamoja na mambo mengine, kufanya uchaguzi wa nafasi kadhaa za uongozi wa kitaifa.
Kutokana na mvutano ulioibuka baada ya Profesa Lipumba kuwasili eneo la mkutano akiongozana na wafuasi wake, uchaguzi ulikwama na mkutano huo kuvunjika.
Chanzo cha vurugu hizo ni wafuasi wa Profesa Lipumba kutaka aruhusiwe kugombea nafasi ya uenyekiti wakati kundi lingine linalounga mkono uongozi kupinga asipewe fursa ya kugombea na kurejea katika nafasi hiyo aliyojiuzulu kwa hiyari yake Agosti 6 mwaka jana.
Vurugu kubwa ziliibuka baada ya wanachama wengi kumpigia Lipumba kura ya kumtaka asiwanie nafasi hiyo kasha mkutano huo kuvunjika.
Siku mbili baadaye Baraza Kuu la Uongozi wa Taifa lilikutana Zanzibar na kuchukua uamuzi huo dhidi ya Profesa Lipumba na wanachama wengine wa CUF.
Uamuzi huo ulipingwa na Lipumba ambaye alikwenda katika Ofisi ya Msajili na kuwasilisha malalamiko, ambayo hatimaye yaliamriwa na Jaji Mutungu mwishoni mwa wiki iliyopita.
Uongozi wa CUF nao umesema kuwa hautambui uamuzi wa Msajili na kwamba maamuzi ya Baraza Kuu la Uongozi ya Agosti 29 yanabakia pale pale na kuandaa mkutano wa kumhoji Lipumba kuhusiana na tuhuma kadhaa juu yake.
Kimsingi, CUF kuna mpasuko ambao unaashiria shari kwa sababu hata Jumamosi iliyopita wakati Profesa Lipumba akirejeshwa ofisini na wafuasi wake, hali haikuwa shwari kutokana na baadhi yao kutumia nguvu kufungua ofisi hizo, kuvunja milango na mageti pamoja na kuwapa kichapo walinzi, licha ya kuwapo askari polisi.
Inasikitisha sana kuona chama hicho cha tatu kwa ukumbwa nchini na kinachotoa ushindani mkubwakwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Zanzibar kikiingia katika mgogoro ambao unaweza kukiathiri.
Sisi tunazishauri pande zote zinazovutana kutumia busara zaidi kwa kuamua kuingiakatika vikao badala ya kutunishiana misuli.
Ikumbukwe kwamba walitumia muda mrefu na rasilimali nyingi kukijenga chama chao, hivyo wasikubali migorogo hiyo ikiathiri chama chao kama ilivyotokea kwa vyama kadhaa vya siasa nchini ambavyo vimepoteza vimedhoofika kutokana na migogoro.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment