Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho
anatarajiwa kuzindua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q 400
zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard
Chamuriho amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo
yamekamilika na uzinduzi huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Kesho kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba
wanahabari na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili
waone utekelezaji wa ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha
usafiri wa Anga hapa nchini”, amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina
ya Bombardier Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja
zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi
za jirani zitakapoanza kazi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment