Hatua
hiyo imekuja baada ya mamlaka hiyo kushindwa kusimamia uendelezaji wa
bonde hilo na kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Septemba 26, 2016) wakati
akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Ikwiriri mkoani Pwani.
Alisema
baada ya mapitio hayo shughuli za mamlaka hiyo zitahamishiwa kwenye
mamlaka nyingine za serikali kwani RUBADA imeshindwa kufanyakazi hiyo
kwa muda mrefu.
“RUBADA wamepewa ardhi lakini wameshindwa kuiendeleza, tutafanya upya mapitio ya kuanzishwa kwake,” alisema.
Akizungumzia
kuhusu Kampuni ya Agro Forestry Plantation inayotaka kujenga kiwanda
cha sukari wiyani Rufiji aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha asilimia 60
ya watumishi watakaowaajiri wawe ni vijana wa wilaya hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri
Mkuu alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium
Lukuvi, kwenda wilayani Rufiji kutatua mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya
ya Mkuranga na Ikwiriri.
Waziri
Mkuu amelitoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa
wananchi wa Ikwiriri kuhusu kutotatuliwa kwa mgogoro huo uliodumu kwa
muda mrefu.
Naye
Mkurugenzi wa halshauri ya wilaya hiyo, Rashidi Salum alimweleza Waziri
Mkuu kuwa, mgogoro huo umeshatatuliwa kwa ngazi ya wilaya hivyo hatua
iliyosalia ni kwa uWaziri wa Ardhi kufika na ramani ili kutoa uamuzi.
0 comments:
Post a Comment