Majambazi
wapatao 10 juzi usiku walivamia magari mawili yaliyobeba
wafanyabiashara waliokuwa wakitokea mnadani na kumuua kwa risasi, dereva
aliyegoma kuwapa fedha na simu.
Dereva huyo, Chrispin Inyangwe (40) alipigwa risasi ya mgongoni alipojaribu kupambana nao.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana eneo la katikati ya vijiji vya
Miula na Kalundi vilivyopo Kata ya Kipande wilayani Nkasi.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema wafanyabiashara hao
walikuwa wakitokea mnadani na walipofika eneo hilo walikuta mawe
yamepangwa barabarani kuzuia magari.
Alisema baada ya kuona mawe
hayo, magari hayo yalilazimika kusimama na ndipo majambazi hao waliokuwa
na silaha za moto, mapanga na marungu walipoibuka na kufyatua risasi
hewani na baadaye kutaka wafanyabiashara hao wasalimishe fedha na simu
zao za mkononi.
Kamanda huyo alisema baadhi ya wafanyabiashara walisalimisha fedha na simu zao, na waliokataa walishambuliwa.
Inasemekana
kwamba Inyangwe ambaye alikuwa dereva wa gari aina ya Mitsubishi Canter
alikaidi kutoa fedha na kutaka kupambana nao, ndipo watu hao waliokuwa
na bunduki aina ya SMG walipomfyatulia risasi iliyompata mgongoni na
kufariki dunia papo hapo.
Kitendo hicho kiliwafanya wafanyabiashara
wengine waliokuwa wakikataa kutoa fedha, kuzisalimisha sambamba na simu
zao, ndipo majambazi hao walipowaachia na kukimbia.
Watu 19
waliojeruhiwa walipelekwa Hospitali ya Mkoa mjini Sumbawanga. Kamanda
Kyando alisema majeruhi 12 waliruhusiwa kurejea nyumbani na wengine saba
wanaendelea na matibabu na kwamba polisi wanaeendelea na msako wa watu
hao.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment