Akizungumza
kwenye sherehe hiyo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
amesema, hadi sasa nchi 60 ambazo zinatoa asilimia 47.5 ya hewa
zinazoweza kusababisha kuongezeka kwa joto duniani zimekubali kujiunga
na makubaliano hayo, na inamaanisha moja kati ya masharti mawili ya
kutekelezwa rasmi kwa makubaliano hayo limetimizwa.
Kwa
mujibu wa kanuni zinazohusika, ni sharti kuwa zaidi ya nchi 55
zilizosaini Mkataba wa mfumo wa mabadiliko ya hali ya hewa ya Umoja wa
Mataifa zikubali kujiunga na makubaliano hayo, ambao utoaji wao wa hewa
zinazosababisha kuongezeka kwa joto duniani unachukua zaidi ya asilimia
55, ili makubaliano ya Paris yatekelezwe rasmi ndani ya siku 30
zinazofuata.
0 comments:
Post a Comment