Waziri
wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Vijana na Watu
Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ametoa siku saba kwa taasisi za serikali,
wizara, kampuni na watu binafsi kuhakikisha wanalipa madeni wanayodaiwa
na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Waziri Mhagama pia
ameziagiza bodi za wadhamini za mifuko mingine ya hifadhi ya jamii,
kuhakikisha zinawashinikiza wadeni wao kulipa madeni yote wanayodaiwa
ili kuiwezesha mifuko hiyo kujiendesha kwa ufanisi zaidi.
Ametoa
tamko hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, alipotembelea miradi
ya nyumba za NSSF iliyopo wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam.
Amemtaka
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Erick Shitindi kuhakikisha uongozi wa
mifuko unampatia ripoti ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika wote
walioshindwa kulipa madeni yao kwa mifuko yao.
“Ninafahamu fika kuna
mikataba ambayo ilisainiwa na pande zote mbili kabla ya kutolewa kwa
hiyo mikopo na makubaliano mengine hivyo naomba basi mikataba hiyo
itumike kufanikisha agizo hili,’’ alisema.
Pia alimuagiza Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini wa NSSF, Profesa Samwel Wangwe kuhakikisha
anampatia ripoti muafaka ya utekelezaji wa agizo hilo.
“Kwa niaba ya
serikali, ninataka kuona kwamba wadaiwa wote wa mifuko hii bila kujali
nafasi zao kiuchumi au kisiasa wanalipa madeni wanayodaiwa…hii lazima
ijumuishe kampuni, wawekezaji na taasisi za serikali,’’ alisisitiza.
Awali,
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema licha ya
mfuko wake kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo majengo,
bado wateja wake wengi hawajalipa madeni wanayodaiwa na mfuko huo
ikiwemo watu binafsi, taasisi za serikali na binafsi wakiwemo pia wale
walionunua nyumba za shirika hilo.
Alisema shirika hilo, bado linadai Sh bilioni 20 kutoka kwa wapangaji wake, deni linalohusisha pia dola za Marekani milioni 1.2.
Alifafanua
kuwa kiasi kingine cha Sh bilioni 86, kinadaiwa kama adhabu kutoka kwa
waajiri walioshindwa kukamilisha makato ya wafanyakazi wao.
Madeni
mengine ni pamoja na deni la Sh milioni 42 na dola za Marekani milioni
35.9 zilizotolewa kama mikopo kwa sekta binafsi mbalimbali huku mkopo
mwingine wa Sh bilioni 38 ulitolewa kupitia Saccs na bado
hazijarejeshwa.
“Hata hivyo, tumeanza kuchukua hatua mahsusi
kulingana na matakwa ya sheria kuhakikisha kwamba madeni yote
yanalipwa,’’ alibainisha Profesa Kahyarara.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment