Msafara wa
makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzani Samia suluhu Hassani
ambao ulikuwa unaelekea wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya rais
Mtwara umepata ajali na kusababisha watu wa nne kujeruhiwa na
kukimbizwa hospitali ya rufaa ligula kwa matibabu zaidi.
Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara
Majeruhi walioumia ni dereva pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.
Inaelezwa
kuwa Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya kiwango cha
kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha
magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha
majeruhi.
Home
News
Slider
Msafara wa Makamu wa Rais wapata ajali,wanne waarifiwa kujeruhiwa na kukimbizwa Hospital.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)




0 comments:
Post a Comment