Binti mmoja kwa jina la Reshma Qureshi ambaye pia alipoteza jicho lake la kushoto kwa kushambuliwa na tindikali ashiriki katika maonyesho ya mtindo jijini New York.
Reshma mwenye umri wa miaka 19 alivalia gauni la asili ya kihindi lililotengenezwa na mwanamtindo Archana Kochhar kutoka India .
Mwanadada huyo yupo shule ya upili mwaka wa pili na anatarajia kujiunga na chuo kikuu baada ya miaka miwili kumalizika .
Akihojiwa na shirika la habari la AFP,Qureshi alielezea jinsi kushiriki katika maonyesho hayo ya mitindo kumemfanya ajihisi kuwa na nguvu zaidi na kumpa matumaini mapya .
Aidha ana azimio la kuwapa matumaini manusura wengine walioshambuliwa kutokana na tindikali.
"Hakuna mtu mwingine anaelewa athari ya kushambuliwa kwa tindikali ila waathirika wenyewe,""Singependa hili kumtokea kwa mtu mwingine."
Mashambulizi kwa kutumia tindikali Asia ya Kusini,Magharibi mwa India na Afrika Kusini ya Sahara hutekelezwa na kulenga hasa wanawake na watoto.
0 comments:
Post a Comment