Rais
wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amewasili Kisiwani
Pemba ambapo na kuzungumza na wananchi wa Pemba katika Mkutano wa
hadhara kwenye
uwanja wa Gombani ya Kale kisiwani humo.
Mara baada ya
kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Pemba kwa Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL), Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli
ameelekea katika kijiji cha Wawi Bigilini kilichopo katika Wilaya ya
Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba ambako amezuru Kaburi la aliyekuwa Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marehemu Dkt. Omar Ali Juma.
Dkt. Magufuli na
Mkewe Mama Janeth Magufuli wameweka mashada ya maua katika Kaburi la Marehemu
Dkt. Omar Ali Juma na wameshiriki Dua ya kumuombea Marehemu iliyoongozwa na
Viongozi wa Madhehebu ya Dini ya Kiislamu na Kikristo.
Akizungumza mara
baada Dua, Rais Magufuli amesema anamkumbuka Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa
ukarimu wake, upendo, kutojikweza, kutobagua watu na kudumisha amani katika
siku zote za maisha yake.
Dkt. Magufuli
ametoa wito kwa Watanzania kudumisha kwa vitendo amani aliyoisimamia Marehemu
Dkt. Omar Ali Juma.
"Mimi najua
huko aliko Marehemu Dkt. Omar Ali Juma anaendelea kuliombea Taifa hili ili hiyo
amani aliyoihubiri katika maisha yake, ili huo upendo aliousimamia katika
maisha yake, ili huo uchapa kazi kwa ajili ya manufaa ya watanzania wote tuweze
kuendeleza kwa mioyo yetu yote" Amesema Rais
Magufuli.
Aidha, Rais
Magufuli amewashukuru Wanafamili wa Marehemu Dkt. Omar Ali Juma kwa uvumilivu
na ustahimilivu wao tangu walipoondokewa na mpendwa wao.
0 comments:
Post a Comment