Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta aliungana na viongozi wengine duniani
kufariji Israel na familia ya rais wa zamani wa Israel Shimon Peres
aliyeaaga dunia mapema siku ya Jumatano.Katika hotuba yake
Kenyatta alielezea kuwa Peres alikuwa kiongozi kamili na mwenye nguvu
aliyeongoza nchi yake kwa utofauti maalum.
Aidha alisema kuwa Peres atakumbukwa kuwa kiongozi aliyekuwa jasiri na pia mwenye aliyependa kuhamasisha amani.
"Israel imempoteza kiongozi muhimu,kwa niaba ya wannchi wa Kenya namuomba Mungu awape familia na Israel nguvu wakati huu mgumu."
Shimon
Peres amefariki akiwa na umri wa miaka 93,atakumbukwa kuwa waziri mkuu
wa Israel mara tatu mfululizo na baadaye kuwa rais kati ya mwaka 2007
hadi 2014.
Peres pia aliwahi kuwa mshindi wa tuzo la amani mwaka 1994 .
Shimon
amefariki hospitalini baada ya kulazwa akikumbana na maradhi ya
kiharusi ambayo yalisababisha kutokwa na damu katika ubongo.
Home
Kimataifa
Slider
Rais Uhuru Kenyatta atuma ujumbe wa rambirambi kwa Israel kufuatia kifo cha Shimon Peres.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment