Romelu Lukaku amefunga magoli matatu yaani hat-trick ndani ya dakika 11, wakati Everton ikiendeleza rekodi yake ya kutofungwa tangu msimu huu uanze na kuibuka na ushindi dhidi ya Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Mshambuliaji huyo raia wa Ubelgiji
alifunga goli la kwanza kwa klabu yake tangu mwezi Machi, kwa mpira
wa kichwa kufuatia krosi ya Idrissa Gueye na kisha kuongeza la pili
kupitia pande la
Yannick Bolasie.
Lukaku alitundika goli la tatu kwa
shuti la chini baada ya kutoka kasi na kuuwahi mpira, na
kuihakikishia Everton ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Sunderland mbayo
haijashinda mchezo wowote wakiwa chini ya kocha David Moyes.
Romelu Lukaku akiruka juu na kutumbukiza mpira wavuni kwa kichwa
0 comments:
Post a Comment