Image
Image

Majaliwa awaomba viongozi wa dini zote kuwahamasisha waumini wao umuhimu wa kulinda Amani.


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amewaomba viongozi wa dini zote kutumia nyumba za ibada kuwahamasisha waumini wao umuhimu wa kulinda na kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Amesema serikali itahakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa nchini ili Watanzania wawe na uhakika wa kuendelea kufanya kazi zao za kuwaingizia kipato na kuwaletea tija.
Waziri Mkuu alitoa rai hiyo wakati akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kumaliza kuswali swala ya Eid El Hajj katika viwanja vya Mwembe Yanga, Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam jana.
“Serikali itaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote nchini. Wito wangu kwa viongozi wa dini msisitize waumini juu ya utunzaji wa amani pamoja na kukemea vitendo viovu ili taifa lizidi kusonga mbele.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment