MUFTI
Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakari Zuberi, amesema matukio ya kupatwa
kwa jua na tetemeko la ardhi yaliyotokea nchini ndani ya siku 10 kati ya
Septemba mosi na Septemba 10, ni ishara ya Mwenyezi Mungu kuwakumbusha
watu wake kutafakari mahali walipokosea na kumrudia.
Akizungumza
katika Swala ya Eid El-Haji ambayo kitaifa ilifanyika Makao Makuu ya
Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Kinondoni Jijini Dar es
Salaam, Mufti Mkuu alisema matukio hayo hayawezi kutokea hivi hivi
isipokuwa Mola kuwakumbusha watu wake kumrudia.
Kutokana na hali hiyo alisema watu wanapaswa kurudi katika nyumba za ibada, kumuomba Mungu awaepushie mambo mabaya wao na nchi kwa ujumla.
“Mtume alisema jua na mwezi ni ishara mbili za kuzibua kudra za Mwenyezi mungu, yaani kuleta mema, hivyo hawezi kuvifanya vipatwe isipokuwa inapotokea hivyo ni ishara ya kuwataka watu wake wamrudie," alisema Sheikh Zuberi.

0 comments:
Post a Comment