SERIKALI haiwezi na wala haina nia ya kufuta michezo nchini kwa
sababu yoyote ile na badala yake itaiendeleza sekta hiyo muhimu kwa
maendeleo ya Taifa hili.
Sambamba na hilo imesema pia haijafuta michezo ya Umitashumta na
Umiseta ila imeahirishwa ili ijipange upya ili wanafunzi wanaofika
kilele cha mashindano hayo wepelekwe kwenye shule maalumu kuendeleza
vipaji vyao.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alikiri
jana kuwa michezo inahitaji uwekezaji mkubwa na kwamba hajaitelekezwa.
Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilolo, Venance
Mwamoto(CCM) aliyedai kwamba hapa nchini michezo ni sawa na mgonjwa
ambaye anahitaji kupelekwa kwenye maombi, hospitali au kwa mganga wa
kienyeji kwa kuwa serikali imeshindwa kuwekeza kuanzia ngazi za chini na
kwa nini haitaki kufufua michezo na kupangia bajeti ya kutosha.
Nape alisema serikali imejipanga kuhakikisha inaboresha michezo kwa
kutenga bajeti pamoja na kutafuta vyanzo vingine vya mapato ikiwemo
michezo ya bahati nasibu ya taifa.
“Nchi zingine zinatumia michezo ya bahati nasibu na sisi tunataka
kutumia mtindo huo, lakini pia nitoe mwito kwa sekta binafsi kuja
kuwekeza katika michezo kwani ni biashara kubwa,” alisema. Katika swali
la msingi Mwamoto alihoji kwa nini serikali isifute michezo?
Akijibu swali hilo la msingi, Nape alisema anamtambua Mwamoto kuwa
mwanamichezo mahiri aliyewahi kuchezea timu za soka za Ligi Daraja la
Kwanza, sawa na Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa sasa, ikiwemo Lipuli ya
Iringa na sasa akiwa kocha wa timu ya Bunge, hivyo haamini kama kweli
anataka serikali kuendeleza sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment