Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Dkt. JULIANA PALLANGYO amesema
serikali imeondoa vikwazo kwa wawekezaji nchini na kuweka mazingira
rafiki ya kufanya biashara ili kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali
nchini.
Akizungumza mara baada ya kufungua semina ya makubaliano ya
Biashara ya Nishati kati ya TANZANIA na NORWAY Dkt PALLANGYO amesema
serikali imeunda sera za kitaifa na sheria mbalimbali ili kuwawezesha
wawekezaji hao kufanya biashara kwa kufuata sheria za nchi.
Naye
Katibu Mkuu wa wizara ya Viwanda na Biashara Prof. JOSEPH MKENDA amesema
mkutano huo utajadili namna wawekezaji kutoka NORWAY wanaweza kuwekeza
nchini TANZANIA husuani katika sekta ya nishati.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment