Serikali
ya Sudan imefanya mashambulizi 30 yanayoshukiwa kuwa ya silaha za sumu
katika eneo la Jebel Marra jimboni Darfur tangu Januari mwaka huu
ikitumia kile watalaamu wamesema ni kemikali ya kusababisha
malengelenge.
Amnesty International imekadiria kuwa karibu watu 250
huenda walifariki kutokana na silaha za kemikali. Shambulizi la karibuni
kabisa lilifanyika Septemba 9 na Amnesty imesema uchunguzi wake
ulizingatia picha za satelaiti, mahojiano na zaidi ya watu 200 na
watalaamu kuchunguza picha zilizoonyesha majeraha.
Mkurugenzi wa
utafiti wa migogoro wa shirika la Amnesty International Tirana Hassan
amesema matumizi ya silaha za sumu ni uhalifu wa kivita ""wakati wa
mashambulizi haya, mamia ya raia walipigwa risasi, maelfu walipoteza
makaazi, na moja ya mambo yanayokasirisha zaidi katika mgogoro wa Darfur
ni kuwa tumepata ushahidi wa kuaminika kuwa serikali ya Sudan imekuwa
ikitumia silaha za sumu dhidi ya raia".
alozi wa Sudan katika Umoja
wa Mataifa Omer Dahab Fadl Mohamed amesema katika taarifa kuwa ripoti
hiyo ya Amnesty "haina msingi wowote kabisa” na kuwa Sudan haimiliki
aina yoyote ya silaha za sumu. Amnesty imesema iliwakabidhi matokeo ya
uchunguzi wake kwa watalaamu huru wa silaha za sumu. "tuliwapa watalaamu
huru wawili ushahidi wote tuliokusanya. Waliuangalia na wakasema kuna
ushahidi wa kuaminika kuwa kumekuwa na matumizi ya aina Fulani ya
kemikali na hasa, kuna uwezekano mkubwa wa matumizi ya kemikali ya
kusababisha malengelenge"
Sudan ilijiunga katika Makubaliano ya Silaha za Sumu mwaka wa 1999 ambapo wanachama hukubali kutotumia silaha za sumu.
Jeshi
la kulinda amani la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, linalofahamika
kama UNAMID, limekuwa Darfur tangu mwaka wa 2007. Usalama bado ni tete
jimboni humo, ambapo makabila yasiyo ya waarabu yanapigana na serikali
ya Khartoum inayoongozwa na waarabu, na serikali inajitahidi kuyadhibiti
maeneo ya mashambani. Karibu watu 300,000 wameuawa Darfur tangu mzozo
huo ulianza 2003, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, wakati watu milioni
4.4 wanahitaji msaada na wengine milioni 2.5 wamepoteza makaazi.
Mahakama
ya Kimataifa ya Jinai ilitoa waranti za kukakamatwa Rais wa Sudan Omar
Hassan al-Bashir mwaka wa 2009 na 2010 kwa tuhuma za uhalifu wa kivita
na mauaji ya halaiki kutokana na operesheni yake ya kuangamiza uasi wa
Darfur.
Home
Kimataifa
Slider
Serikali ya Sudan imefanya mashambulizi 30 yanayoshukiwa kuwa ya silaha za sumu
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment