Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA kinampongeza rais John Pombe Magufuli na rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein kwa uteuzi wa viongozi na hasa wanawake ambao wameteuliwa kwa kuwa na imani kuwa wataongeza ufanisi wa kazi katika nafasi zao mbalimbali za maamuzi kwa maslahi ya jamii na taifa zima.
Uteuzi huo ambao umefanyika hivi karibuni, Chama cha TAMWA kimepata viongozi ambao ni wanachama wake wanne walioteuliwa
na rais Magufuli pamoja na rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi ambapo TAMWA tunajivunia na kuwaomba wote walioteuliwa
wajitume kwa bidii zaidi ili wawe mfano kwa wengine.
Wanachama
wa TAMWA walioteuliwa pamoja na nafasi zao ni Mahfoudha Alley Hamid
(Ummie) ambaye amekuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya shirika la
magazeti ya serikali Zanzibar, Maryam Hamdan – Mwenyekiti wa baraza la
sanaa na sensa ya filamu na utamaduni Zanzibar, Nasra Mohamed Juma –
Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), Rahel Mhando –
Katibu Tawala Wilaya mpya ya Kigamboni.
Aidha;
TAMWA inawapongeza Rais na makamu wake Samia Suluh Hassan kwa kuona
umuhimu wa kuongeza wanawake katika nafasi za ngazi za juu za uongozi
kwa kuwa mwanamke ana mchango mkubwa katika kutetea maslahi na maendeleo
ya nchi.
TAMWA
inaamini kuwa, katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo nchini, uteuzi
wa wanawake katika nafasi za juu ni fursa itakayowezesha kuondolewa kwa
mapungufu yaliyopo kiuongozi ili kuwepo usawa na haki kwa watanzania
wote – wanawake na wanaume.
Aidha;
TAMWA inaamini kuwa bado wapo wanawake wanawake wengi wenye uwezo ambao
mchango wao unahitajika katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo hapa
nchini.
Edda Sanga
Mkurugenzi Mtendaji
0 comments:
Post a Comment