Serikali
imetakiwa kuhakikisha kuwa na itikadi thabiti katika kutekeleza sera
zilizowekwa na waasisi wa taifa katika kuondoa ujinga, maradhi na
umasikini ili kuleta maendeleo haraka kwa wananchi wake
Hayo
yamezungumzwa na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba, katika
Mhadhara wa tatu wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere ambao ulikuwa
unazungumzia elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika.
Jaji Warioba
amesema kuwa sasa Tanzania imekosa sera madhubiti ya kiitikadi na
kutegemea zaidi matukio na watu na kusema endapo kutakuwa na sera
itikadi madhubuti itasaidia kulipeka taifa mbele katika maendeleo.
Amesema
vijana wengi wanaimba wimbo wa kutaka maendeleo kwa kuimba wimbo wa
kufuta ujinga, maradhi na umasikini bila kujua waasisi wa taifa
walitumia mbinu gani katika kufanikisha kuleta maendeleo kwa wananchi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment