Zaidi ya shilingi MILIONI HAMSINI na magunia KUMI NA MOJA ya mahindi
vimepatikana katika harambee iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji
Tanzania –TBC, kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi
la SEPTEMBA KUMI mkoani KAGERA.
Harambee hiyo iliyofanyika jijini DSM imetangazwa moja kwa moja na
TBC ambapo watazamaji na wasikilizaji wamepata fursa ya kuchangia kwa
njia ya simu.
Akizindua harambee hiyo iliyoandaliwa na TBC, Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, NAPE NNAUYE amelipongeza shirika hilo kwa
ubunifu na kuwataka watanzania kuungana pamoja kuchangia waathirika wa
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani KAGERA.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. AYUB RIOBA amesema TBC
inachangia kwa kuhamasisha wananchi kuchangia kupitia Televisheni na
radio.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment