Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amezindua mpango mkakati na mradi wa
maboresho ya huduma za mahakama TANZANIA na kuboresha utoaji wa huduma
pamoja na kuongeza kasi ya kusikiliza na kesi zilizoko mahakamani
ili kupunguza tatizo la mashauri kukaa muda mrefu mahakamani bila
kutolewa maamuzi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo mkoani PWANI Waziri Mkuu
MAJALIWA amesema utaratibu huo ukizingatiwa utasadia wananchi kutumia
muda mfupi kufuatilia kesi zao mahakamani.
Awali akimkaribisha waziri mkuu KASIM MAJALIWA kuzindua mpango huo
jaji mkuu wa Tanzania MOHAMED CHANDE OTHMANI amesema mahakama imejipanga
kuimarisha utoaji wa huduma na kujenga mahakama za wilaya katika
wilaya ,mikoa.
Uzinduzi wa mpango mkakati mradi wa maboresho ya huduma za mahakama
TANZANIA umeenda pamoja na uwekeji wa jiwe la msingi ujezi wa mahakama
ya wilaya ya KIBAHA inayojengwa kwa utaalamu mpya ambao ujenzi wake
hutumia gharama nafuu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment