Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ihungo.
Serikali imetenga shule SABA kwa ajili ya kuwahamishia wanafunzi
waliokuwa wanasoma katika shule za sekondari za IHUNGO na NYAKATO ambazo
zimefungwa baada ya kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea
Septemba 10 mkoani KAGERA.
Akizungumza mkoani KAGERA, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI, GEORGE SIMBACHAWENE amezitaja
shule watakazohamishiwa wanafunzi hao kuwa ni KAHORORO, UMUMWANI,
BIHARAMULO, NYAKAHURA, KISHOJU, NYAILIGAMBA na chuo cha KKKT BUKOBA.
Waziri SIMBACHAWENE amesema wanafunzi hao wanatarajiwa kurejea katika
shule zao za awali ifikapo JANUARY TISA mwakani baada ya ujenzi wa
shule hizo kukamilika.
Amewashauri wanafunzi kutembelea tovuti ya TAMISEMI ili kujua shule walizopangiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment