Image
Image

Tusisingizie umaskini kuwadhulumu watoto


Katika kipindi cha hivi karibuni, kumejitokeza vitendo vingi vya kuwadhalilisha watoto kwa kuwabaka, kuwanajisi, kuwalawiti, kuwatesa, kuwaua bila hatia.

Matukio hayo yote inatokana na sababu zisizo na msingi zikiwemo za ushirikina na kutafuta utajiri, vitendo ambavyo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.
Miaka mitatu iliyopita kulijitokeza wimbi la mauaji kwa walemavu wa ngozi, hasa kwa mikoa ya Kaskazini, mauaji ambayo yalishinikizwa na imani za kishirikina, jitihada za polisi pamoja na jamii iliyokasirishwa na vitendo hivyo zilisaidia kupunguza kasi ya mauaji hayo, ingawa matukio kama hayo yameripotiwa kutokea.
Mashirika na taasisi mbalimbali za haki za watoto zimeguswa na mateso wanayopata watoto na kuwasababishia ulemavu, unyonge na kutojiamini katika maisha yao.
Yapo matukio mengi mengine ambayo yanahusu udhalilishwajki watoto ambayo huishia katika suluhu za kifamilia kwa misingi ya kukwepa aibu katika jamii.
Watoto wamekuwa wakitendewa vitendo vibaya bila ya jamii kuchukua hatua za kisheria kwa visingizio vya kulinda heshima ya wazazi pamoja na kujenga mahusiano mema miongoni mwa familia zinazotuhumiana.
Suala hilo kwa hakika limerudisha nyuma jitihada za kukomesha ukatili dhidi ya watoto nchini.

Umaskini uliokithiri miongoni mwa jamii yetu ni moja ya vyanzo vinavyokwaza jitihada za kupambana na unyanyasaji na ukatili kwa watoto.Mara nyingi Wazazi wanapotambua kuwa mtoto wao katendewa vitendo vihovu, wakaahidiwa malipo ya fidia jambo ambalo ni hatari.
Zipo sheria za mwaka 2009, Sura ya pili kipengere cha 5 (1), 5 (2) na 13 zinazolinda haki za watoto ambapo pamoja na mambo mengine vinaelea kwa undani haki na ustawi wa mtoto, inaeleza mtoto ni nani na mambo gani anapaswa kufanyiwa.
Wazazi tuamkeni tuwalinde watoto kwa hali yoyote na tusithubutu kudhulumu haki zao kwa kisingizio cha umasikini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment