Akizungumza na waandishi wa habari 30 Septemba
jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema
hawataji tarehe nyingine ili kukwepa maandalizi ya Serikali yanayoweza
kuwadhuru wanachama wao.
Mh.Mbowe
amesema sababu ya kuahirisha Ukuta ni kutokana na kukosa ushirikiano
kutoka kwa viongozi wa dini waliowaomba waahirishe ili wakazungumze na
viongozi wa Serikali.
Ambapo Operesheni hiyo ilipangwa kuzinduliwa Septemba mosi nchini kwa maandamano na mikutano ya hadhara kama maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema, baada ya chama hicho kukumbwa na vikwazo kadhaa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara.
ikumbukwe kwamba Siku moja kabla ya kufanyika kwa operesheni hiyo ya UKUTA ya Septemba Mosi, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliutangazia uma wa watanzania kwamba wanasitisha maandamano hayo kwa mwezi hadi 1 Octoba 2016, ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kuzungumza na na Rais John Magufuli na Serikali yake ili kuona namna itakavyo kuwa.
0 comments:
Post a Comment