Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT) Prof. Benno Ndulu amesema pato la taifa
limeongezeka kwa asilimia 6.76 katika kipindi cha nusu ya kwanza ya
mwaka 2016 (Januari hadi Juni) ukilinganisha na kipindi hicho mwaka
jana ambapo nusu ya kwanza ya mwaka 2015 pato la taifa liliongezeka kwa asilimia 5.7.
Prof. Ndulu amezitaja Sekta zilizoongoza kwa kukuza pato hilo kuwa ni
Uchukuzi na uhifadhi mizigo iliyochangia asilimia 17.4, uchimbaji madini
na gesi asilimia 13.7 sekta ya mawasiliano asilimia 13 na sekta ya
fedha na bima kwa asilimia 13.
Makusanyo ya ndani yameongezeka kwa asilimia 34.
0 comments:
Post a Comment