Mfalme wa Music wa Singel Tanzania - MSAGA SUMU.
UKWELI MCHUNGU,USHEMEJI WA MSAGA SUMU.
Nidhahiri kwamba kila kukicha muziki aina ya Singeli unakuwa huku lengo likiwa nikuvuka mipaka na kufika katika mataifa mengine ya njee ya Tanzania.
Muziki huu wa Singeli huwezi kuutaja bila wazo ama picha ya Msaga Sumu kukujia akilini mwako hata kidogo, kutyokana na kwamba sehemu mbali mbali Amekuwa akifanya poa haswa kwenye vigodoro ambapo wengi wamekuwa wakifurahi na uimbaji wake.
Ukweli Mchungu licha ya wengi ambao huibukia Music wa Singeli, lakini Msaga Sumu nimoja ya Msanii Nguli na Mfalme wa Singeli ambaye amekuwa kivutio cha wengi kwenye music huu.
Vibao vya Msaga Sumu ni vingi mnoo kuvitaja humu vitachukua muda, lakini Ukweli Mchungu kwa Wimbo wake wa UNANITEGA SHEMEJI, umekuwa ukipendwa mnoo kila sehemu ya nchi yetu haswa maeneo ya uswahilini lakini kwa jinsi pia alivyo urekodi tofauti na ilivyokuwa ikifanyika siku za usoni.
UNANITEGA SHEMEJI - umefanya mapinduzi ya Music ambapo baadhi ya wasanii wamepata wasaa wakumuimba Shemeji huyu wa Msaga Sumu, huku wakisema Tunakulaga hainaga USHEMEJI na pia nao kufanya vizuri katika sanaa.
Mapitio yenye umakini kwenye wimbo wa msaga sumu wa UNANITEGA SHEMEJI, ukiusikiliza na kuutizama inaonesha namna gani SHEMEJI wanavyowatega wadogo wa kaka, lakini msaga sumu anapinga kutembea na shemejiye huku akieleza kuwa katika familia yao wapo wawili tu sasa akitembea na shemejiye si hatari kwake licha ya visa anavyo vifanya shemeji.
Shemeji alishawahi kuimba nguli wa Music wa enzi hizo Baraka Mwishehe, akisema Shemeji Shemeji huku unazima taa, wimbo ambao mpaka hivi leo unatamba na kusikika maridadi ulimwengu wa leo.
Music huu umewavuta wasanii wakubwa nao kubadilisha ladha ya Music na Kuimba Singel, Ambapo Mbunge wa Mikumi na Msanii wa Hip hop nchini Tanzania Prof.Jay amekubali Music wa Singel huku akiupigia chapuo wa kuhakikisha kuwa unafika mbali na akiwa anawasisitizia wasanii wanaoingia kuimba Singel na ambao washakuwa ndani ya Music huo wa Singel kuhakikisha wanafanya music huo unaheshimika kitaifa na kimataifa.
Kauli za Prof.Jay mara kadhaa akikaririwa na vyombo vya habari anawasisitizia wasanii wa Singel kuimba music huo kwa utanashati, tofauti na unavyochukuliwa na jamii kuwa ni mkusic wa kihuni tu jambo ambalo sio kama waimbaji wa singel watakuwa katika umoja wenye kuhakikisha Music huo unakuw wa watanashati.
Wasanii wa Singel wapo wengi mno na wanahitaji kupata nafasi ya kuimba na kutoka kama wengine waliopata majina licha ya kuwa swali lililopo je kwa kuwa Music huu unapigiwa chapuo kuika mbali kila mmoja anaona nimwepesi kuimba tu ama nini dhamira ya waimbaji hawa?.
Mawazo ya wanajamii wanafikiri kuwa Music huu uwe somo kwa vijana kupitia tungo zenye kuelimisha pasi na tungo zenye kuhamasisha uovu na mambo mengine kusudi uweze kuweka heshima na kushindana na music mwingine uliopo sokoni na kutambulika mara dufu ya ulipo.
Bado tunasema UKWELI MCHUNGU, Msaga Sumu anaonesha kuwa na Mvuto mnoo katika mitaa mbalimbali kupitia Music wa Singel tofauti na Baadhi ya tunao waona, kutokana na maneno ya wananzengo wenyewe wa uswahilini kukiri kuwa mkali wao ni Msaga Sumu.
Itaendelea wk ijayo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment