Wadau
wa maendeleo na wananchi wamesema uelewa mdogo kuhusu umuhimu wa vyeti
vya kuzaliwa na mlolongo wa kuvipata ni sababu za Watanzania zaidi ya
milioni 30 kutokuwa navyo.
Juzi,
gazeti hili lilichapisha habari iliyomkariri Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita), Emmy Hudson aliyesema
kuna changomoto kubwa katika usajili wa vizazi na vifo kwa sababu watu
hawaoni umuhimu wake, mfumo wa ukoloni na ubovu wa miondombinu.
Hudson
ambaye alifanya mahojiano maalumu na gazeti hili, alisema kuwa asilimia
13 ya Watanzania ndiyo waliosajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa.
Alisema hiyo ina maana kwamba karibu Watanzania milioni 39 kati ya
milioni 44 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2012 sawa na
asilimia 87, hawajaandikishwa.
Wakizungumzia
kauli hiyo, baadhi ya wadau wa maendeleo na wananchi wa kawaida
walisema sababu ni kutokuwa na uelewa juu ya umuhimu wa kuwa na vyeti
vya kuzaliwa, huku baadhi ya wananchi wakidai mlolongo wa kupata vyeti
hivyo ni mrefu.
Akizungumza
kwa njia ya simu, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za
Binadamu (LHRC), Dk Hellen-Kijo Bisimba alisema: “Ukimwambia mtu kuhusu
cheti anasema cha nini?”
Alisema watu wanashindwa kutambua cheti cha kuzaliwa ni kitambulisho muhimu kwao.
Mkurugenzi huyo alisema ni haki kwa kila mzazi anapopata mtoto, kuhakikisha anafuatilia hadi anapata cheti hicho.
Dk
Bisimba alisema hata baadhi ya watu wenye vyeti vya kuzaliwa
walilazimika kuvitafuta kutokana na mahitaji ya kisheria hususan katika
kupata hati za kusafiria nje ya nchi na kuandikisha watoto shule.
Kaimu
Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Rabikira Mushi alisema mahitaji ya
kisheria yameongeza idadi ya Watanzania wanaoomba vyeti hivyo.
Mkazi
wa Tabata Relini, Richard Marijani alisema siyo kila mwananchi
anafahamu umuhimu wa vyeti hivyo na kwamba, wengi wao hulazimika
kuvitafuta wanapotaka hati za kusafiria.
advertisement
0 comments:
Post a Comment