Image
Image

Mwanachama mpya Julian King ateuliwa kuwa msimamizi wa muungano wa usalama wa baraza la Umoja wa Ulaya

Julian King kutoka Uingereza ameteuliwa kuwa kama mwanachama mpya wa kusimamia muungano wa usalama wa baraza la Umoja wa Ulaya.Mwenyekiti wa baraza la Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker alitoa maelezo na kutangaza kuteuliwa kwa Julian King kwenye nafasi hiyo mpya ya usimamizi wa muungano wa usalama.
Julian King atahudumu katika wadhifa huo na kukamilisha muhula wake tarehe 31 Oktoba mwaka 2019.
Hapo awali, Jonathan Hill ambaye ni mmoja wa wanachama waliokuwa na wadhifa mkuu katika Umoja wa Ulaya aliwahi kutangaza kujiuzulu kama mwanachama wa baraza la EU kufuatia uamuzi wa Uingereza wa kutaka kujitenga na muungano.
Baraza la Umoja wa Ulaya linajumuisha wanachama 28 wanaowakilisha nchi zote zilioko ndani ya muungano huo.
Julian King pia aliwahi kuhudumu kama balozi wa Uingereza mjini Paris nchini Ufaransa kabla ya kuteuliwa katika wadhifa mpya wa baraza la Umoja wa Ulaya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment