Vitendo
vya ukatilitili wa kijinsia kwa watoto vimeendelea kuongezeka kwa kasi
nchini katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu ambapo
zaidi ya watoto 2,570 wa kike na kiume wamelawitiwa na kubakwa.
Akizungumza
katika sherehe za maadhimisho ya miaka 21 ya Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu (LHRC) yaliyofanyika jana katika Makao makuu ya watoto
yaliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC
Helen Kijo-Bisimba alisema idadi hiyo ni kubwa ukilinganisha na ya mwaka
jana.
Hata hivyo, Mama Bisimba alisema kwa mujibu wa Msemaji wa
Jeshi la Polisi, takwimu hizo zinaweza kuwa ndogo kutokana na kesi
nyingi za ubakaji na ulawiti kwa watoto kutoripotiwa polisi kwa sababu
ya mila na desturi za maeneo mengi nchini.
“Ripoti ya Jeshi la Polisi
kupitia dawati la jinsia kati ya Januari na Machi 2016 inaonyesha
matukio ya watoto kubakwa na kulawitiwa yakiendelea kuongezeka kutoka
180 hadi 1765 hayo ni matukio yaliyotolewa taarifa katika vituo
mbalimbali vya polisi nchi nzima ukilinganisha na matukio 1585 mwaka
2015. Hata hivyo waliohusika na matukio hayo wameonekana wakirandaranda
bila kuchukuliwa hatua za kisheria, ” alisema.
Alisema ripoti hiyo
inaonyesha kuwa kesi 1,203 zipo katika hatua ya upelelezi, 822 zipo
mahakamani na watuhumiwa 234 wamekwisha hukumiwa.
“Pia utafiti
uliofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto kwa
kushirikiana na Tanzania kitengo cha ustawi wa jamii unaonyesha kati ya
watoto 10 wa kike 4 wamebakwa, na kati ya watoto 10 wa kiume 3
wamelawitiwa zaidi ya mara tatu. Utafiti huo unaonyesha kwa ujumla kuwa
watoto wa kike na wa kiume 6 walifanyiwa ukatili huo na watu ndani ya
familia,” alisema.
Bisimba alisema asilimia 49 ya ukatili hufanyika
nyumbani, 23 hufanyika njiani wakati wa kwenda shule au kurudi, na
asilimia 15 hufanyika shuleni. Pia ripoti hiyo ya UNICEF inaonyeaha
kuwepo kwa matukio ya watoto kulawitiana na kubakana wenyewe kwa wenyewe
kutokana na kuvizoea vitendo hivyo.
LHRC imeitaka serikali kupitia
Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na
Wizara ya Katiba na Sheria kuifanyia marekebisho sheria ya mtoto na
kutilia mkazo malezi bora kwa watoto ikiwemo kuweka kipengele
kitakachotoa adhabu kali kwa familia itakayoshindwa kutoa malezi bora
kwa mtoto.
LHRC inayoshughulika na utetezi wa sheria na haki za binadamu ilianzishwa Septemba 26, 1995.
Home
News
Slider
Vitendo vya ukatilitili wa kijinsia kwa watoto vimeendelea kuongezeka kwa kasi nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment