Image
Image

Watu wamiminika RUJEWA kushuhudia tukio la Kupatwa kwa Jua.

Wananchi wakiwa wamekusanyika katika kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua katika Kijiji cha Rujewa wilayani Mbarali Mkoani Mbeya muda mfupi kuanzia sasa.
Katika tukio hilo takribani watanzania 500 watashuhudia, likiwa tukio la kipekee linalo tokea kila baada ya miaka 15.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza Tanzania kutokea tukio hilo tangu Aprili 18, 1977 na kwamba tukio kama hilo la kihistoria linatarajiwa kutokea tena nchini Mei 21, 2031.
Mbali ya Rujewa ambako wataona kupatwa kwa jua kwa asilimia 97 sawa na miji ya Makambako, Masasi, Mbeya, Tunduru, Njombe na Sumbawanga, miji mingine ambayo itaona tukio hilo kwa ukaribu zaidi wa asilimia 96 ni Katavi, Nachingwea na Songea ikifuatiwa na Kigoma, Iringa, Mtwara na Lindi.
Katika sehemu mbalimbali hadi muda huu hali imeshaanza kubadilika kwa ishara tosha kuwa shughuli hiyo ya kihistoria ya kupatwa kwa jua ndio inakolea nazi, ambapo wataalam wa masuala ya anga wamelichagua eneo la Rujewa kwaajili ya kuratibu mabadiliko hayo ya kupatwa kwa jua yanayotazamiwa kuanza mwendo wa saa tano  mpa saa nane mchana. Tafsiri halisi ya kupatwa kwa jua:Kupatwa kwa jua kunatokea kama dunia ,mwezi na jua kukaa kwenye mstari  mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua.
Tutawapa kinachoendelea eneo hili,Pia tembeleeni ukurasa wetu wa Faceebok https://www.facebook.com/tambararehalisi/kufahamu kinachojiri kwa wakati.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment