Mapema asubuhi ya leo, watu wanaodaiwa kuwa ni Madalali wa Shirika
la nyumba la Taifa (NHC) wamefika ofisi za Gazeti la kila siku la
Tanzania Daima zilizopo katika makutano ya Mtaa wa Mkwepu na Indraghand
na kuwatolea vyombo vyote nje kufuatia deni la muda mrefu la kodi ya
pango wanalodaiwa bila kulipwa. Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Neville
Meena amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa wako kwenye
Msukosuko mkubwa sana sasa ila wanafanya jitihada za kukabiliana na hali
hiyo ili kuhakikisha uzalishaji wa gazeti unaendelea kufanyika kama
kawaida.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Gazeti hilo wakiwa nje ya Ofisi huku wakitafakari namna ya kufanya.
Vyombo vya Ofisi hiyo vikiwa nje.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment