Mkutano
wa Wakuu wa nchi na Serikali umemalizika katika mjini Mbabane Swaziland
ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi muhimu na nyeti ya
Siasa, Ulinzi na USalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-
SADC- (SADC Organ On Politisc, Defence and Security Cooperation) ambapo nchi ya Angola imeteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa asasi hiyo.
Jukumu
kubwa la asasi hiyo litakuwa ni kuangalia masuala yote yanahusiana na
Siasa, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC huku changamoto kubwa
ikiwa ni namna ya kutafuta suluhu ya kudumu hususani katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na
Lesotho.
Akizungumzia
mambo muhimu yaliyojiri kwenye Mkutano huo wa 36 wa SADC mjini Mbabane -
Swaziland, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt John Magufuli amesema mkutano huo umekuwawa mafanikio
makubwa na amehimiza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika
kuwaletea wananchi maendeleo.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa nchi wanachama wa SADC kwa
sasa zinatakiwa kuongeza juhudi katika kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi haraka kama hatua ya kujenga ustawi bora wa wananchi wa kanda hiyo.
Kuhusu
Mpango wa Mfalme wa Swaziland wa III wa kujenga Chuo Kikuu cha SADC
nchini mwake kabla ya mkutano ujao wa SADC hapo mwakani chuo ambacho kwa
kuanzia kitatoa ufadhili wa masomo ya Sayansi,Ugunduzi na Utafiti kwa wanafunzi wanaotoka kwenye nchi wanachama wa SADC,
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema mpango huo ni mzuri na
utasaidia kutoa wataalamu wengi hasa wanasayansi katika ukanda wa SADC
na serikali ya Tanzania inaunga mkono mkakati huo.
Kuhusu Tanzania kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa nchi za SADC, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dkt
Augustine
Mahiga amesema Tanzania itahudumu katika asasi hiyo kwa mwaka MMOJA na
anaimani kuwa changamoto za kisiasa zilizopo katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Lesotho zipatiwa ufumbuzi.
Mkutano
wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC pia umeiteua nchi ya Swaziland
kuwa mwenyekiti wa SADC na Jamhuri ya Afrika Kusini imeteuliwa kuwa
Makamu Mwenyekiti wa SADC.
Katika
mkutano huo wakuu wa nchi na serikali wametia saini rasimu za maboresho
ya mikataba mbalimbali ya jumuiya hiyo ikiwemo mkataba wa kuboresha
itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa
siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais MbabaneSwaziland.
Home
News
Slider
Tanzania yateuliwa kuwa mwenyekiti wa asasi muhimu na nyeti ya siasa,ulinzi na usalama SADC.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment