Mwanasiasa mkongwe na waziri wa zamani wa serikali ya Kenya William Ole Ntimama ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 86.Vyanzo
vya habari nchini Kenya vimearifu kwamba Ole Ntimama alifariki katika
nyumba yake iliyoko kaunti ya Narok usiku wa Alhamisi.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na kamanda wa polisi wa kaunti ya Narok, Ole Ntimama aliwahi kupokea matibabu ya kiafya mwezi uliopita.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliyetambulika kama kiongozi wa jamii ya Wamaasai, aliwahi kuwa mbunge wa eneo Narok Kaskazini kati ya mwaka 1988-2013.
Ole Ntimama pia aliwahi kuhudumu kama waziri wa utawala katika ofisi ya rais kati ya mwaka 2004-2007 na baadaye kuhamishwa katika wizara ya utamaduni kati ya mwaka 2008-2013.
Ole Ntimama alistaafu siasa rasmi mwezi Septemba mwaka 2013.
Ole Ntimama alikuwa ni mmoja wa wanasiasa wakongwe walioahidi kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2017 alipozuru ikulu pamoja na wazee wa jamii ya Wamaasai.

0 comments:
Post a Comment