Umoja
wa Mataifa umezihimiza kuwepo kwa utulivu nchini Gabon baada ya fujo
kuzuka kuhusiana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.
Baraza
la Usalama la umoja huo limetoa wito kwa wagombea wakuu na wafuasi wake
kujizuia kufanya uchokozi na kutatua mzozo wa sasa kupitia njia za
kisheria.
Maafisa wa usalama kufikia sasa wamewakamata watu zaidi ya elfu moja baada ya siku ya pili ya maandamano ya wafuasi wa upinzani.
Upinzani unadai Rais Ali Bongo aliiba kura wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi.
Rais Bongo amesisitiza kwamba alishinda kwa njia halali na kuutaja ushindi wake kuwa ushindi wa watu wa Gabon.
Amesema kuna kundi ndogo la watu wachache waliotaka kutwaa madaraka na ambao wameshindwa.
Matokeo
ya uchaguzi yalitangazwa Jumatano alasiri na kumpatia Bw Bongo ushindi
kwa 49.8% ya kura, akifuatwa na Bw Ping aliyepata 48.2 % ya kura, kura
zilizowatenganisha zikiwa 5,594.
Bw Ping alisema uchaguzi huo ulijaa udanganyifu na "hakuna ajuaye" hasa nani alishinda.
Upande
wa Bw Ping unasema takwimu kutoka ngome za rais huyo zinaonyesha
asilimia 99 ya wapiga kura walijitokeza. Ameomba takwimu za wapiga kura
kutoka kila kituo zitolewe wazi.
Bw Bongo aliingia madarakani mwaka wa 2009, baada ya kifo cha babake aliyekuwa ameongoza taifa hilo tangu 1967.
Kabla ya kuingia katika siasa, Ping aliwahi kuhudumu kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment